KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Gerardo Martino amejiuzulu wadhifa huo siku chache baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Chile katika fainali ya michuano ya Copa America. Katika taarifa yake Martino amesema amefikia hatua hiyo kwasababu ya uhaba wa maamuzi kutoka katika uongozi wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-AFA na matatizo yaliyopo katika kuteua kikosi kwa ajili ya michuano ya Olimpiki. Kocha huyo raia wa Argentina ameiongoza timu hiyo kutoka Agosti mwaka 2014 baada ya kuacha kuinoa Barcelona. Nyota wa kutegemewa wan chi hiyo Lionel Messi ambaye alikosa penati katika mchezo wa fainali, alitangaza kustaafu baada ya mchezo huo akidai kuwa inaumiza sana kutokuwa bingwa.
No comments:
Post a Comment