Friday, July 15, 2016

WOLFSBURG WAMKOMALIA DRAXLER.

MKURUGENZI wa michezo wa Wolfsburg, Klaus Allofs amedai kuwa Julian Draxler atabakia katika klabu hiyo kipindi hiki cha kiangazi. Taarifa kutoka Ujerumani zilikuwa zikidai kuwa Wolfsburg walikuwa wako tayari kuuza zaidi ya wachezaji 10 katika kipindi hiki cha usajili na kuna uwezekano wa kuvutiwa na ofa ya euro milioni 60 kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22. Wolfsburg walimaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Bundesliga msimu uliopita na klabu hiyo tayari imekiri kuwa Andre Schurrle anaweza kuondoka kufuatia kuwindwa na Borussia Dortmund. Lakini Allofs amesema Draxler hatakuwa mchezaji mojawapo atayeuzwa katika kipindi hiki cha kiangazi.

No comments:

Post a Comment