MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa beki wake Gabriel Paulista natarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu. Kwa upande mwingine kiungo Jack Wilshere naye anatarajiwa kuukosa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Jumapili hii kutokana na majeruhi ya goti. Gabriel aliumia katika mchezo wa mwisho wa Arsenal wa maandalizi ya msimu mpya dhidi ya Manchester City Julapili iliyopita lakini alikaririwa katika mitandao wa kijamii jana akidai kuwa majeruhi yake sio makubwa sana. Hata hivyo, Wenger leo amesema Gabriel atakaa nje kwa wiki sita mpaka nane kutokana na vipimo alivyofanyiwa.

No comments:
Post a Comment