Wednesday, August 10, 2016

RANIERI ATWISHWA MIAKA MINNE LEICESTER.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ligi Kuu ambao unatarajiwa kumalizika mwaka 2020. Ranieri ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati alipochukua nafasi ya Nigel Pearson kiangazi mwaka jana, aliiongoza Leicester kutwaa taji hilo katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha. Akihojiwa katika tovuti ya klabu hiyo, Ranieri ambaye pia amewahi kuzinoa Chelsea, Juventus na Monaco, amesema pindi alipozungumza na wamiliki na kujua mipango yao mara moja alifahamu hapo ndio mahali anahitaji kukaa kwa kipindi kirefu. Ranieri aliendelea kudai kuwa amefurahi na anajivunia kuwa sehemu ya klabu hiyo kwa miaka mingi ijayo. Naye ofisa mkuu wa klabu hiyo Susan Whelan amesema klabu hiyo inajivunia kumuongeza mkataba Ranieri kwani ni kocha ambaye kutokana na weledi na uzoefu wake amewasaidia kuvuka malengo waliojiwekea kwa msimu wake wa kwanza.

No comments:

Post a Comment