Saturday, August 6, 2016

BOSI WA LEICESTER AFANYA KUFURU.

MMILIKI wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha amefanya kufuru kwa kuwanunuliwa wachezaji wote wa timu hiyo magari ya kifahari kama alivyowaahidi wakishinda taji la Ligi Kuu msimu uliopita. 
Uwanja wa King Power eneo la maegesho jana lililikua limetawaliwa na magari aina ya BMW 18s ambalo kila moja linakadiriwa kugharimua kiasi cha paundi 105,000. Zawadi ya magari hayo ambayo kwa jumla inadaiwa kufikia kiasi cha paundi milioni mbili, ni mahsusi kwa ajili ya ubingwa waliotwaa Mwezi Mei mwaka huu. 
Kwasasa Leicester wanajiandaa na mchezo wa ngao wa hisani utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Wembley dhidi ya Manchester United.

No comments:

Post a Comment