KLABU ya Inter Milan imetangaza rasmi Mholanzi Frank de Boer kuwa kocha wao mpya akichukua nafasi ya Muitaliano Roberto Mancini aliyetimuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. De Boer alisafiri kwenda jijini Milan jana, kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho wake kabla ya klabu hiyo kutangaza rasmi leo uteuzi wake. De Boer mwenye umri wa miaka 46 ambaye aliacha kuinoa Ajax Amsterdam mwishoni mwa msimu uliopita alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda kuzinoa klabu za Ligi Kuu za Southampton na Everton kabla ya nafasi hizo hazijazibwa. Akihojiwa Inter De Boer atakuwa na chini ya wiki mbili ya kusajili wachezaji zaidi kabla ya msimu wa Serie A haujaanza ambapo wao wataanza kwa kucheza na Chievo Agosti 21 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment