Thursday, August 4, 2016

CITY WATUPA NDOANO KWA CHIPUKIZI WA COLOMBIA.

KLABU ya Manchester City inadaiwa kukaribia kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Marlos Moreno. City wanatarajiwa kuilipa klabu ya Atletico Nacional ya Colombia kiasi cha paundi milioni 4.75 kwa ajili ya chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19. Hata hivyo, City wanatarajia kumpeleka kwa mkopo mchezaji huyo katika klabu ya Deportivo La Coruna. Moreno atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Pep Guardiola wiki hii kufuatia ujio wa Leroy Sane kutoka Schalke na Gabriel Jesus kutoka Palmeiras.

No comments:

Post a Comment