Thursday, August 4, 2016

USAJILI WA SAKHO KWENDA WEST BROM WAKWAMA.

UHAMISHO wa mshambuliaji wa West Ham United Diafra Sakho kwenda West Bromwich Albion ka kitita cha paundi milioni 15 unadaiwa kusitishwa baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo vya afya huko The Hawthorns. Inaaminika kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Senegeal hakushindwa vipimo vya afya lakini inadaiwa asingekuwa fiti kwa ajili ya mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu. Sakho mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 15 katika mechi 44 za ligi alizoichezea West Ham katika kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini amekuakisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara. Ujio wake West Brom ulizua tetesi kuwa klabu hiyo inaweza kumuuza mshambuliaji wake Saido Berahino mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekuwa akiwindwa na klabu za Crystal Palace na Stoke City.

No comments:

Post a Comment