MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesema mwamuzi alifanya uamuzi sahihi kwa kutotoa adhabu dhidi ya mshambuliaji Diego Costa baada ya kumparamia kipa wa West Ham United Adrian. Costa alikuwa tayari ameshalimwa kadi ya njano wakati alimpomvamia Adrian mguuni katika kipindi cha pili. Mwamuzi wa mchezo huo Anthony Taylor hakutoa kadi nyingine ya njano na Costa kuendelea na kuja kuisaidia Chelsea kushinda mabao 2-1. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Conte amesema mwamuzi hakuona vyema na kuongeza alichoona yeye ni Costa kwenda kumpa kashikashi kipa na baadae kujaribu kujizuia ili asimuumize. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Costa hakudhamiria kumchezea hovyo kipa huyo ila alienda kwenye tukio akiwa amechelewa.
No comments:
Post a Comment