KLABU ya Liverpool imekataa ofa ya paundi milioni 30 kutoka kwa Crystal Palace kwa ajili ya mshambuliaji wao Christian Benteke. Palace walikuwa wanataka kutanguliza kiasi cha paundi milioni 23 mbele huku zingine zilizobakia wakitaka kulipa kwa awamu kufuatia ofa yao ya awali ya paundi milioni 25 nayo pia kukataliwa. Benteke mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akikosa nafasi ya kucheza Liverpool toka Jurgen Klopp alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Octoba mwaka jana, akianza katika mechi nane za ligi pekee. Nyota huyo alijiunga na Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 32.5 Julai mwaka 2015 chini ya meneja wa zamani Brendan Rodgers na kufanikiwa kufunga mabao 10. Palace wanadaiwa kutuma ofa hiyo baada ya kumuuza winga wake Yannick Bolasie kwa paundi milioni 25 kwenda kwa mahasimu wao wa Ligi Kuu Everton jana.

No comments:
Post a Comment