KLABU ya Burnley imetangaza kufanya usajili wa Steven Defour kutoka Anderlecht kwa ada iliyovunja rekodi ya timu hiyo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka mitatu na Burnley baada ya Anderlecht kuthibitisha makubaliano kati ya klabu hizo mbili wiki iliyopita. Klabu hiyo ya Ligi Kuu imethibitisha kumsajili kiungo huyo kwa ada kubwa zaidi katika historia yao lakini hawakuiweka wazi ni kisasi gani. Taarifa ziliendelea kudai Defour anategemewa kuja kuleta uzoefu wake kwa timu hiyo ili kuhakikisha wanabaki katika Ligi Kuu.

No comments:
Post a Comment