HATIMAYE klabu ya Yanga imeamua kwa kauli moja kumsimamisha uanachama katibu wa Baraza la Wazee wa klani hiyo mzee Yahya Akilimali licha ya kuwasilisha utetezi wake. Hatua hiyo imefikiwa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa matawi uliofanyika katika ofisi za klabu hiyo zilizopo mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam. Mzee Akilimali anatuhumiwa kwa kile kilichoitwa kumkashifu mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Mehboob Manji, baada ya kudai kuwa kiongozi huyo amekuwa akijiamulia mambo yeye mwenyewe bila kumshirikisha mtu yeyote. Katika utetezi wake mzee Akilimali alikiri kusema maneno hayo lakini aliomba radhi ka wanawayanga wote na kuonyesha kujutia kile alichosema kuhusu kiongozi huyo. Hata hivyo, utetezi wa Akilimali haukufua dafu mbele ya viongozi hao wa matawi ambao kwa kauli moja wlaiamua kumsimamisha uanachama kwa muda usiojulikana. Manji alitangaza nia ya kujiuzulu nafasi yake ya mwenyekiti akidai amekuwa akiandamwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wakituhumu na kuponda kauli yake ya kutaka kupewa timu hiyo kwa kipindi cha miaka 10.

No comments:
Post a Comment