Monday, August 15, 2016
SEVILLA YATOTA KWA BARCELONA.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez amesisitiza bado hawajatwaa taji la Super Cup ya Hispania pamoja na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla katika mchezo wao wa mkondo kwanza uliochezwa jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay alifunga bao lake mapema katika kipindi cha pili kabla ya Munir El Haddadi hajafunga la pili akimalizia pasi murua ya Lionel Messi. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Suarez amesema mchezo bado haujaisha kwani ingawa ilikuwa ni muhimu kushinda mchezo wao wa kwanza. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kipindi cha pili wlaicheza vyema na kupata ushindi huo muhimu na sasa ni wajibu wao kuhakikisha wanafanya hivyo tena katika mchezo wa marudiano. Barcelona wanatarajia kurudiana na Sevilla Agosti 17 mwaka huu katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Camp Nou.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment