Monday, August 15, 2016

ANCELOTTI ATWAA TAJI LA KWANZA AKIWA NA BAYERN.



MENEJA mpya wa Bayern Munich, carlo Ancelotti amefanikiwa kutwaa taji lake la kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kuifunga Borussia Dortmund katika Super Cup ya Ujerumani. Arturo Vidal ndio aliyeanza kuifungia Bayern bao la kuongoza kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Thomas Muller hajaongeza la pili na kuzamisha jahazi la Dortmund. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ancelotti amesema ulikuwa mchezo mgumu na wapinzani wao Dortmund walicheza vizuri sana lakini mambo yaliwaendea vyema baada ya mapumziko na kuwapa hali ya kujiamini zaidi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kikosi chake tayari kiko imara kwa imara kwa ajili ya kutetea taji lao msimu ujao. Msimu mpya wa Bundesliga unatarajiwa kuanza Ijumaa ya Agosti 26, wakati Bayern watakapokwaana na Werder Bremen.

No comments:

Post a Comment