Monday, August 15, 2016
WENGER ATUPIA LAWAMA SAFU YAKE YA ULINZI.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ukosefu wa uzoefu katika safu ya ulinzi ndio suala lililoigharimu timu hiyo kwa kufungw amabao 4-3 nyumbani na Liverpool jana. Wenger aliongeza pia kuchelewa kurejea kwa wachezaji wake nyota baada ya michuano ya Ulaya nako kulisababisha mambo kuwa magumu zaidi kwa upande wao. Lakini hatahivyo, meneja huyo amesema hakuna sababu ya kutaharuki baada ya timu yake kuzomewa mara baada ya filimbi ya mwisho na kuongeza kuwa mchezaji yeyote mpya atakayemsajili ni lazima awe bora. Akihojiwa Wenger amesema kikosi chake kilicheza vyema katika kipindi cha kwanza na ilikuwa bahati mbaya kwao kuruhusu bao la kusawazisha muda mchache kabla ya mapumziko. Wenger aliendelea kudai kuwa toka wafungwe bao lile hawakuweza kurejea mchezo tena na kukosekana kwa wachezaji wazoefu katika safu ya ulinzi ilipelekea hali yao kuwa mbaya zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment