Sunday, August 14, 2016

MAMILIONI YAWASUBIRIA WACHEZAJI WA NIGERIA WAKITWAA DHAHABU OLIMPIKI.

KILA mchezaji katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ameahidiwa kiasi cha dola 30,000 sawa na shilingi milioni 65,490,000 kama wakishinda medali ya dhahabu katika michuano ya soka ya Olimpiki inayondelea jijini Rio de Janeiro. Daktari mashuhuri wa upasuaji raia wa Japan, Katsuya Takasu ndio aliyetangaza nia yake hiyo, huku pia akidai atatoa kiasi cha dola 20,000 kama wakishinda medali ya fedha na dola 10,000 kama wakishinda medali ya shaba. Akihojiwa Takasu amesema amesoma kuhusu matatizo ya kifedha yanaoikabili timu hiyo na akaona ni muhimu akafanya jambo kuchangia. Takasu aliongeza kuwa hafanyi hivyo kwa ajili ya kutafuta umarufu ila anataka kuwapa vijana moyo na ari zaidi ya kufanya vyema katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment