NAHODHA wa Leicester City, Wes Morgan amesema kipigo cha kushtusha walichopata kutoka kwa Hull City jana ni kipimo tosha kuwa sasa wanapaswa kuanza kutetea taji lao. Leicester ambao walipoteza michezo mitatu pekee kati ya 38 ya Ligi Kuu waliyocheza msimu uliopita, jana walijikuta wakitandikwa mabao 2-1 na Hul ambao ndio kwanza wamepanda daraja msimu huu. Akihojiwa Morgan amesema walijitahidi lakini hawakuwa bora kama wapinzani wao hivyo Hull walistahili ushindi waliopata. Nahodha huyo aliendelea kudai kuwa wanachotakiwa ni kujifunza kutokana na makosa waliyofanya ili kuhakikisha mchezo ujao wanakuwa bora zaidi. Naye meneja wa Leicester Claudio Ranieri alikiri kuwa sababu kubwa iliyochangia kufungwa kwao ni kutocheza kwa umoja kama walivyozoea.

No comments:
Post a Comment