MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema hana tatizo lolote na kipa Joe Hart pamoja na kumuacha katika kikosi chake cha kwanza kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu. Kipa wa kimataifa wa Argentina, Willy Caballero ndio aliyeanza katika mchezo huo wa jana ambao City walishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland huku Hart akiwa benchi. Akiulizwa ni jinsi gani kipa huyo wa kimataifa wa Uingereza alivyochukulia taarifa za kuwekwa benchi, Guardiola amesema alizichukulia vizuri kwani anamheshimu sana kipa huyo lakini kwa mchezo wa jana aliamua kumtumia Caballero. Guardiola aliendelea kudai kuwa ana kikosi kizuri na mwishoni ni lazima atoe maamuzi ya mchezaji atakayemtumia kwa jinsi alivyoona ubora wake.

No comments:
Post a Comment