MSHMABULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Olimpiki wakati wenyeji Brazil walipoibaruza Colombia mabao 2-0 na kutinga hatua ya nusu fainali ya soka la wanaume. Nyota huyo alifunga bao lake hilo kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 12 ya mchezo kabla ya Luan hajaongeza la pili baada ya mapumziko. Brazil sasa wanatarajiwa kucheza Honduras Jumatano ijayo ijayo katika hatua hiyo baada ya timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini. Nusu fainali nyingine itazikutanisha Ujerumani dhidi ya wawakilishi pekee wa Afrika katika michuano hiyo Nigeria. Nigeria walitinga hatua hiyo baada ya kuichapa Denmark mabao 2-0, wakati Ujerumani wao waliibugiza Ureno mabao 4-0.

No comments:
Post a Comment