KIUNGO wa Manchester United aliyevunja rekodi ya dunia ya usajili Paul Pogba amefungiwa kucheza mechi moja ya ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Bournemouth Jumapili hii. Adhabu hiyo ilibainishwa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA, ikihusisha adhabu aliyokuwa amepata wakati akiwa katika klabu ya Juventus. Katika taarifa yake FA wamesema Pogba alilimwa kadi mbili za njano msimu uliopita katika mechi za Serie A ambapo matokeo yake ni kufungiwa mchezo mmoja, hivyo anahama na adhabu yake hiyo nchini Uingereza. Nyota huyo aliyesajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 89 tayari alishazua wasiwasi wa kutocheza mechi hiyo kutokana na kutokuwa fiti sawasawa. Mchezo wake wa kwanza kwa United sasa unaweza kuwa Ijumaa ya Agosti 22 wakati watakapocheza na Southampton.

No comments:
Post a Comment