Friday, August 12, 2016

MIMI SINA KIBURI - IBRAHIMOVIC.

MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa tuhuma za kuwa ana kiburi sio kweli na kudai kuwa yeye ni mtu anayejiamini sana. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden ambaye anatarajiwa kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Bournemouth Jumapili hii, anatajwa kuwa mtu anayependa kujikweza na kuwadharau wapinzani wake. Lakini Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34 amesema kuwa kujiamini kwake ndio kulikomfanya kutwaa mataji manne ya ligi katika nchi nne tofauti. Ibrahimovic aliendelea kudai kuwa hadhani kama ana kiburi bali anajiamini na uhakika wa kile anachofanya ndio maana amepata mafanikio yote hayo.

No comments:

Post a Comment