Friday, August 12, 2016

KOCHA ARGENTINA APATA MATUMAINI YA MESSI KUREJEA.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Argnetina, Edgardo Bauza amesema ana matumaini ya kumshawishi Lionel Messi kubadili uamuzi wake wa kustaafu baada ya kukutana na nyota huyo mshindi wa tuzo tano za Ballon d’Or. Bauza amesema amekuwa na mazungumzo mazuri na nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 wakati walipokutana jana jijini Barcelona. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa walizungumza masuala ya soka na ana matumaini mazuri ingawa hayupo kichwani kwake kujua anawaza nini. Bauza amesema katika kikao chake na Messi nyota mwingine wa nchi hiyo Javier Mascherano naye alikuwepo. Bauza ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo Agosti mosi mwaka huu, anatarajiwa kutangaza chake leo kwa ajili ya mchezo wao ujao wa kufuzu Kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment