BEKI wa Sunderland Lamine Kone amemwambia meneja wake David Moyes kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27, ambaye anawindwa na Everton, alijiunga na Sunderland Januari mwaka huu na kuisaidia timu hiyo kutoshuka daraja msimu uliopita. Kone amesema uamuzi wake huo umekuja baada ya klabu kushindwa kumpa mkataba wenye maslahi bora zaidi kama walivyomuahidi. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Kone alithibitisha kuzungumza na Moyes na kumueleza mipango yake ya baadae kuwa anataka kuruhusiwa kuondoka na kwenda kutafuta changamoto nyingine. Sunderland wanatarajia kuanza kampeni zao za Ligi Kuu kwa kucheza na Manchester City kesho.

No comments:
Post a Comment