Friday, August 12, 2016

HAKAN SUKUR ASAKWA KWA UHAINI.


MWENDESHA mashitaka wa Uturuki anayechunguza jaribio la mapinduzi lililoshindwa ameagiza kukamatwa kwa mwanasoka nguli wa zamani wa nchi hiyo Hakan Sukur. Ukaguzi katika nyumba zake mbili zilizopo magharibi wa nchi hiyo, na maofisa wamesema anakabiliwa na kesi kwasababu ya tuhuma za kujihusisha na kikundi cha kigaidi kinachotumia silaha. Sukur ambaye pia ni mbunge wa zamani wa chama tawala cha AK, anajulikana kwa kuunga mkongo kikundi kilichoshindwa mapinduzi ya kuipindua serikali iliyopo madarakani. Miezi michache iliyopita Sukur alihamia nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment