MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani, Lebrone James anatarajiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi msimu ujao wa NBA baada ya kukubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 100 na timu ya Cleveland Cavaliers. Wakala wake amesema James anategemea kusaini kiasi cha dola milioni 31 kwa msimu ujao kiasi ambacho kitapanda mpaka dola milioni 33 kwa msimu 2017-2018. James aliiongoza Cavaliers timu ya mji anaotoka, kutwaa taji lao la kwanza la michuano ya NBA msimu uliopita baada ya kujiunga nao mwaka 2014. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, james amesema anashukuru kwa nafasi hiyo waliyompa ya kuweza kutetea taji lao walilotwaa msimu uliopita.

No comments:
Post a Comment