Friday, August 12, 2016

WENGER AKATAA KUMJADILI MUSTAFI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa kujadili hatua za klabu hiyo kumuwania beki wa Valencia Shkodran Mustafi baada ya wakala wa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani kusisitiza makubaliano yameshafikiwa. Lakini akiongeza na wana habari kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool, Wenger alikataa kabisa kujadili suala hilo. Akihojiwa kushuaiana na hilo Wenger amesema hawezi kuwaambia lolote kwani kwasasa hayuko sana katika masuala ya usajili kwasababu ya mchezo muhimu walionao katika kipindi cha saa 48 zijazo. Wenger aliendelea kudai kuwa wana kikosi imara kwa ajili ya mchezo huo pamoja na kuwapoteza beki wake watatu wa kati kwasababu ya Laurent Koscielny naye pia hayuko tayari kwa ajili ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment