NYOTA wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na Pepe wamerejea mazoezini baada ya kumaliza likizo zao walizopewa kufuatia kushinda taji la michuano ya Ulaya wakiwa na Ureno. Ronaldo alikuwa akihofiwa kukosa mwanzo wa msimu kufuatia kutolewa nje katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo dhidi ya ufaransa baada ya kuumia goti. Hata hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 sambamba na Pepe wote wamerejea mazoezini pamoja wakiwa tayari kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Real Sociedad Agosti 21 mwaka huu. Wachezaji wote wawili jana walikosa mchezo wa Super Cup ya UEFA ambapo Madrid walishinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Sevilla, lakini walifanya mazoezi ya ndani pamoja na kukimbia.

No comments:
Post a Comment