Monday, August 1, 2016

GATTUSO AIKIMBIA KLABU YA SERIE B.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Italia, Gennaro Gattuso amejiuzlu kuifundisha klabu ya daraja la pili ya Pisa ya Italia muda mfupi kabla ya kuanza msimu mpya kwasababu ya kushindwa kuelewana na viongozi. Gattuso aliiongoza klabu hiyo inayotoka katika mji wa Tuscan, Italia kupanda daraja mpaka Serie B msimu uliopita na alishatishia kujiuzulu kama uongozi usingetimiza matwaka yake. Mara baada ya kuinoa timu hiyo kwa wiki kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya, Gatusso ameamua kujiuzlu sababu kubwa ikiwa mazingira mabovu ambayo yanamfanya kushindwa kufanya kazi yake vyema. Gattuso enzi zake alitumia kipindi kirefu akiitumikia klabu ya AC Milan kabla ya kuamua kutundika daruga zake na kuhamia masuala ya ukocha miaka minne iliyopita.

No comments:

Post a Comment