Monday, August 1, 2016

MAN CITY YAKARIBIA KUMNASA CHIPUKIZI WA SCHALKE.

KLABU ya Manchester City inadaiwa kukaribia kukamilisha usajili wa Leroy Sane kutoka klabu ya Schalke ya Ujerumani kwa ada inayotajwa kufikia paundi milioni 37. Klabu hiyo ya Bundesliga imetangza leo kuwa kiungo huyo hajajiunga nao katika kambi ya mazoezi nchini Austria na badala yake alisafiri kuelekea Manchester. Meneja mpya wa City, Pep Guardiola alithibitisha Julai 21 mwaka huu kuwa anataka kumsajili Sane. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 aliisaidia nchi yake ya Ujerumani kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya mwaka huu, akiwa ameitwa kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment