BEKI wa Barcelona, Javier Mascherano anatarajiwa kukosa mchezo wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Real betis kutokana na majeruhi ya msuli wa paja aliyopata. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alipata majeruhi hayo wakati wa mchezo wa Super Cup dhidi ya Sevilla jana. Mascherano alitolea nje na kupelekea Barcelona ambao walikuwa wameshamaliza wachezaji wote watatu wa akiba, kumaliza mchezo huo wakiwa na 10 uwanjani. Hata hivyo, mabao mawili ya Arda Turan na moja la Lionel Messi yalitosha kuwahakikishia ushindi wa mabao 3-0 na kuwafanya kutwaa taji hilo kwa jumla ya mabao 5-0 katika michezo miwili waliyokutana.
No comments:
Post a Comment