KIUNGO mpya wa Manchester United, Paul Pogba amesema ni wakati muafaka kwa yeye kurejea Old Trafford baada ya kukamilisha usajili wake uliovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 89.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anarejea baada ya kupita miaka minne, wakati alipoondoka United kwenda Juventus kwa kitita cha paundi milioni 1.5 mwaka 2012. Pogba ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano, aliongeza kuwa klabu hiyo ndio sahihi kwake kupata mafanikio ambayo anayategemea.

Naye meneja wa United Jose Mourinho amesema nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kuja kuwa mchezaji muhimu kwa klabu hiyo kwa miaka 10 ijayo. United inatarajia kuilipa Juventus euro milioni 105 kwa ajili ya Pogba, kuongeza paundi milioni tano kulingana na kiwango na gharama zingine ikiwemo euro milioni tano kama Pogba akisaini mkataba mpya. Usajili huo unaupia ule wa paundi milioni 85 ambao Real Madrid waliwalipa Tottenham Hotspurs kwa ajili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale mwaka 2013.

No comments:
Post a Comment