Thursday, August 25, 2016

SAMATTA ALIVYOIPELEKA GENK MAKUNDI EUROPA LEAGUE.



MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta jana amefanikiwa kuingoza vyema klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Katika mchezo huo Samatta alifunga bao muhimu la kuongoza katika dakika ya kwanza ya mchezo katika ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Genk dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia. Ushindi huo waliopata katika Uwanja wa Luminus Arena umewafanya kutinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza uliofanyika huko Zagreb. Ratiba ya makundi ya michuano hiyo inatarajiwa kupangwa baadae leo huko jijini Monaco, Ufaransa.

No comments:

Post a Comment