Saturday, August 6, 2016

WENGER ADAI PESA SIO TATIZO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa fedha sio tatizo kwa klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili lakini amedokeza kuwa itabidi aanze na wachezaji alionao kwa ajili ya mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu wiki ijayo. Wenger bado amekuwa akitaka kusajili beki wa kati na mshambuliaji baada ya kufanya usajili mmoja mkubwa kiangazi hiki kwa kumchukua kiungo Granit Xhaka. Arsenal wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuwawania mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette na beki wa Valencia Shkodran Mustafi lakini Wenger amesema baada ya kuibugiza Viking mabao 8-0 katika mchezo wa kirafiki, kuwa tatizo sio bei bali wachezaji. Meneja huyo amesema siku zote fedha imekuwa sio tatizo kama unalipa kwa aina ya mchezaji unayemuhitaji.

No comments:

Post a Comment