BEKI wa zamani wa klabu za Real Madrid, Tottenham Hotspurs na Newcastle United, Jonathan Woodgate anatarajiwa kuchukua kibarua cha kuwa skauti wa Liverpool. Woodgate mwenye umri wa miaka 36 alitundika daruga zake mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuisaidia timu ya nyumbani kwao ya Middlesbrough kupanda daraja katika Ligi Kuu. Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kufanya kazi ya kuitafutia vipaji Liverpool katika nchi za Hispania na Ureno. Woodgate alisajiliwa Madrid akitokea Newcastle kwa kitita cha paundi milioni 13.4 mwaka 2004, na kuungana na Waingereza wenzake David Beckham na Michael Owen huku akicheza sambamba na wakali wengine akiwemo Zinedine Zidane, Ronaldo na Luis Figo.

No comments:
Post a Comment