KLABU ya Villarreal imetangaza rasmi kumtimua kocha wake Marcelino Garcia Toral muda mfupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa La Liga. Marcelino ambaye anaondoka sambamba na msaidizi wake Ruben Uria, amekuwa akiinoa timu hiyo toka mwaka 2013 lakini anaondoka kufuatia kutoelewana na uongozi wa klabu. Kuondoka kwake kumekuja wakati kipindi kibaya wakati ambapo Villarreal inajiandaa kuikaribisha AS Monaco katika Uwanja wa El Madrigal kwa ajili ya mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano ijayo. Villarreal ambao walimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga msimu uliopita wamekuwa wakitajwa kumuwania kocha wao wa zamani Manuel Pellegrini ambaye yuko huru baada ya kuondoka Manchester City.

No comments:
Post a Comment