Thursday, August 11, 2016

SUNDERLAND YASAJILI WAWILI KUTOKA MAN UNITED.

KLABU ya Sunderland imefanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka Manchester United Paddy McNair na Donald Love wote kwa pamoja wakiwachukua kwa kitita cha paundi milioni 5.5. Wachezaji wanaocheza nafasi ya ulinzi wamepewa mikataba ya miaka minne wakiungana na meneja wao wa zamani wa United david Moyes ambaye amechukua nafasi ya Sam Allardyce JUlai mwaka huu. Klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake na kuongeza kuwa nyota hao wenye umri wa miaka 21 wanakuwa usajili wa tatu na wa nne kwa toka Moyes amechukua mikoba ya kuinoa Sunderland. Naye Moyes aliwasifia wachezaji hao akidai kuwa bado wanachipukia lakini wana uwezo mkubwa wa kuimarika zaidi chini yake.

No comments:

Post a Comment