MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Adnan Januzaj anataka kuondoka moja kwa moja katika klabu hiyo baada ya kuachwa katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mkataba wake unamalizika 2018 na klabu hiyo ilikuwa ikiangalia uwezekano wa kumpeleka kwa mkopo. Hata hivyo, Januzaj ameonyesha kuchukizwa kwa jinsi anavyofanyiwa hivyo kumfanya afikirie kuondoka moja kwa moja. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na Sunderland ambayo inanolewa na meneja wa zamani wa United David Moyes. Inaaminika kuwa Januzaj hakutaarifiwa kama atakuja kunyang’anywa jezi namba 11 aliyokuwa akivaa na badala yake amepewa Antony Martial huku mshambuliaji mpya Zlatan Ibrahimovic akichukua namba tisa iliyokuwa ikivaliwa na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Januzaj sasa amepewa jezi namba 15 na amepewa maelekezo ya kufanya mazoezi na kikosi cha akiba cha timu hiyo.

No comments:
Post a Comment