MENEJA wa Juventus, Massimiliano Allegri ameonyesha kuwa na imani na kikosi chake, akikumbusha kuwa bado wana muda wa kuimarika kutoka katika sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya Sevilla. Mabingwa hao wa Serie A walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini walishindwa kuzitumia vyema katika mchezo huo uliofanyika jijini Turin jana usiku. Lakini pamoja na kushindwa kupata ushindi katika mchezo wao huo wa kwanza wa kundi H, Allegri amekitaka kikosi chake kubaki na mawazo chanya. Allegri amesema hakuna mechi rahisi katika michuano hiyo, hivyo hawapaswi kuanza kutembea vichwa sasa kwani bado wana muda mwingi wa kujipanga na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. Mechi ijayo Juventus wanatarajiwa kusafiri kuifuata Dinamo Zagreb ya Croatia Septemba 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment