Thursday, September 15, 2016

USHINDI WAMPA JEURI RANIERI.



MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri anadhani bao la mapema walilopata lilikuwa muhimu katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge jana. Mabingwa hao wa Ligi Kuu walikwenda katika mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kutandikwa mabao 4-1 na Liverpool Jumamosi iliyopita, matokeo ambayo yamewafanya kuporomoka mpaka nafasi ya 16 katika msimamo. Hata hivyo, mambo yalikuwa tofauti katika mchezo huo kwa bao la mapema la Marc Albrighton aliyetumia mwanya kwa kujichanganya kwa mabeki wa Brugge kabla ya Riyadh Mahrez hajafunga mabao mengine mawili na kuwahakikishia alama zote tatu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ranieri amesema ilikuwa muhimu kushinda kwoa haswa baada ya kipigo cha Liverpool na bao la mapema walilofunga liliwafanya wajiamini zaidi. Leicester sasa wanatarajiwa kucheza na FC Porto katika mchezo unaofuata wa kundi G Septemba 17 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment