MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mazungumzo yanatarajiwa kuanza kujaribu kuwashawishi Mesut Ozil na Alexis Sanchez kuongeza mkataba mpya. Ozil na Sanchez wote kwa pamoja wamebakisha miaka miwili katika mikataba yao ya sasa, lakini Wenger amepania kuwaongeza ili waendelee kubakia. Nyota wa kimataifa wa Ujerumani Ozil alisajili kwa kitita kilichovunja rekodi ya klabu cha paundi milioni 42.5 kutoka Real Madrid mwaka 2013, wakati Sanchez yeye alijiunga akitokea Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 35 mwaka 2014. Akihojiwa kuelekea mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris saint-Germain, Wenger alithibitisha taarifa hizo kuwa mazungumzo yataanza rasmi karibuni.
No comments:
Post a Comment