KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza, Eric Dier amesaini mkataba mpya wa miaka mitano Tottenham Hotspurs ambao utamuweka hapo mpaka mwaka 2021. Nyota huyo wa zamani wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Spurs mwaka 2014 na amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha cha Spurs chini ya meneja Mauricio Pochettino. Spurs ilithibitisha taarifa za kumuongeza mkataba nyota huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter. Kiwango kikubwa alichoonysha Dier akiwa na Spurs msimu uliopita kilipelekea kuitwa katika kikosi cha Uingereza kilichoshiriki michuano ya Ulaya na kufanikiwa kufunga bao moja la mpira wa adhabu katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Urusi.
No comments:
Post a Comment