KLABU ya Everton imetoa msaada wa paundi 200,000 kuisaidia familia ya shabiki wa Sunderland mwenye umri wa miaka mitano kulipia gharama za matibabu ya saratani nchini Marekani. Kiasi cha paundi 700,000 kinatarajiwa kukusanywa zitakazomsaidia Bradley Lowery, ambaye alikuwa mwanasesere wakati Sunderland ilipotandikwa mabao 3-0 dhidi ya Everton jana usiku katika Uwanja wa Light. Kufuatia kugundua tatizo la kijana huyo, Everton waliamua kumsaidia kiasi hicho cha fedha ili kuunga mkono juhudi za kuokoa maisha yake. Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter klabu hiyo ilimtakia kila la heri Bradley katika safari yake hiyo ya kimatibabu.
No comments:
Post a Comment