MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Burkina Faso, Ben Idrissa Derme amefariki dunia amefariki dunia wakati wa mchezo wa Kombe la Ufaransa akiwa na klabu yake ya daraja la chini ya AJ Biguglia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, alipata shambulio la moyo mapema katika kipindi cha pili kwenye mchezo huo wa mzunguko wa tatu kwa klabu hiyo. Watu wa huduma ya kwanza walijitahidi kumuhudumia Derme uwanjani lakini walishindwa kumsaidia kupumua tena. Derme ameichezea Burkina Faso mechi nne na amekuwa akicheza katika ligi za chini nchini Ufaransa na pia Moldova.
No comments:
Post a Comment