MSHAMBULIAJI wa Nice, Mario Balotteli amedai kuwa uamuzi wake wa kujiunga na Liverpool ulikuwa mbaya kuwahi kufanya katika maisha yake. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia amefunga mabao manne katika mechi 28 alizoichezea Liverpool toka aliponunuliwa kwa paundi milioni 16 kutoka AC Milan mwaka 2014. Balotelli pia amefanikiwa kufunga bao moja pekee katika mechi 20 za Serie A alizoichezea Milan kwa mkopo msimu uliopita kabla ya kujiunga na Nice akiwa mchezaji huru. Akihojiwa mara baada ya kufunga mabao mawili na kuisaidia Nice kushinda mabao 3-2 dhidi ya Marseille jana, Balotelli amesema ukiacha mashabiki na baadhi ya wachezaji ambao alikuwa akielewana nao, hakuipenda klabu kabisa klabu hiyo. Balotelli aliendelea kudai kuwa amekuwa na makocha wawili Liverpool, wa kwanza Brendan Rodgers na mwingine kwa kipindi kifupi Jurgen Klopp lakini hakuna hata mmoja aliyemsaidia.
No comments:
Post a Comment