MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simone amesisitiza hana tatizo lolote kw akikosi chake kukosolewa kwasababu ya kutoshinda mchezo wowote wa La Liga mpaka sasa. Atletico ambao walikuwa wakishindi wa pili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, wametoka sare katika mechi zao mbili za mwanzo na kuwafanya kuachwa nyuma kwa alama nne na mahasimu wo Barcelona na Real Madrid. Akihojiwa kuelekea mchezo wao wa ugenini dhidi ya Celta Vigo mwishoni mw wiki hii, Simeone amesema ni haki watu kukosoa wakati ambao hawapati matokeo na kukiri kuwa wanatakiwa kujiimarisha zaidi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba wanakabiliwa na mchezo mgumu ugenini dhidi ya Celta Vigo lakini watajitahidi kushinda.
No comments:
Post a Comment