Wednesday, September 14, 2016

CEFERIN NDIO RAIS MPYA UEFA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemchagua Aleksander Ceferin kuwa rais mpya wa shirikisho hilo. Ceferin ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka la Slovenia, alipata kura 42 katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika jijini Athens, ikiwa ni 29 zaidi ya mpinzani wake Michael van Praag wa Uholanzi. Rais huyo mpya mwenye umri wa miaka 48, anachukua nafasi ya nguli wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Michel Platini ambaye alijiuzulu baada ya kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo mwaka jana. Ceferin ataitumikia nafasi hiyo kwa kipindi chote cha Platini kilichobakia mpaka mwaka 2019. Akihojiwa mara baada ya uchaguzi huyo, Ceferin amesema ni heshima kubwa lakini pia kuna changamoto kubwa hivyo atajitahidi kadri ya uwezo wake kuweza kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi.

No comments:

Post a Comment