KLABU ya Crystal Palace imethibitisha kukamilisha uhamisho wa kiungo wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini akiwa kama mchezaji huru. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amekuwa mchezaji huru toka alipoachwa na Arsenal kiangazi hiki, akiwa amecheza mechi 24 kwa klabu hiyo msimu uliopita. Akihojiwa mara baada ya kukamilisha uhamisho huo, Flamini amesema Palace ni klabu yenye malengo na wachezaji wakubwa hivyo anadhani safari yake hiyo mpya itakuwa na mafanikio. Flamini aliongeza kuwa alizungumza na Alan Pardew kuhusu uhamisho wake na mazungumzo yao yalichangia kwa kiasi kikubwa kuvutiwa kujiunga nao.

No comments:
Post a Comment