Thursday, September 8, 2016

STAM ATHIBITISHA GYAN KUSHINDWA VIPIMO VYA AFYA.

MENEJA wa Reading, Jaap Stam amethibitisha klabu hiyo kusitisha uhamisho wa Asamoah Gyan baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana kushindwa vipimo vya afya. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland mwenye umri wa miaka 30, alikuwa akitarajiwa kujiunga na Reading akitokea klabu ya Shanghai SIPG ya China. Lakini badala yake Gyan amejiunga na klabu ya Al Ahli ya Falme za Kiarabu kwa mkopo baada ya klabu hiyo inayoshiriki ligi ubingwa kujitoa. Akiulizwa kama Gyan alifeli vipimo, Stam amesema ni kweli kwani mchezaji huyo hakuwa fiti wakati alipofanyiwa vipimo.

No comments:

Post a Comment