Thursday, September 8, 2016

PAYET KUREJEA UWANJANI JUMAMOSI HII.

MENEJA WA West Ham United, Slaven Bilic amesema kiungo Dimitri Payet anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu katika mchezo dhidi ya Watford Jumamosi hii. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeruhi ya goti, mara mwisho aliichezea West ham akitokea benchi katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Chelsea mwezi uliopita. Payet amefunga mabao 12 katika mashindano yote kwa West Ham msimu uliopita baada ya kujiunga nao akitokea Olympique Marseille, Juni mwaka jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa pia alifunga mabao matatu katika michuano ya Ulaya iliyofanyika katika ardhi ya nyumbani mapema kiangazi hiki.

No comments:

Post a Comment