TIMU ya taifa ya El-Salvador imedai kukataa hongo ili wapange matokeo ya kushindwa katika mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 waliocheza dhidi ya Canada baadae leo. Katika mkutano na wanahabari, wachezaji wa timu hiyo walitoa sauti ya iliyorekodiwa ya mtu wanaedai alitaka kuwapa hongo hiyo. Katika mchezo huo utakaofanyika jijini Vancouver, Canada ni lazima waifunge El Salvador na wakiwa na matumaini Mexico iichape Honduras katika mzunguko wa mwisho wa kundi A, ili waweze kuweka hai matumaini yao ya kufuzu. El Salvador wao hawawezi kufuzu katika mechi hizo za mwisho za makundi.

No comments:
Post a Comment